Ipo haja ya kuwashirikisha washika dau wote wa amani pamoja na wakaazi wa eneopana la bonde la ufa katika juhudi za kufanikisha amani katika bonde la Kerio.
Gavana wa kaunti ya Nandi Stephen Sang akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini KCCB la kuzindua kampeni ya amani kaskazini mwa bonde la ufa, gavana Sang amesema kuwa serikali pekee haiwezi kukomesha vita hivyo, akikariri haja ya kushirikisha wakaazi, makanisa pamoja na washikadau mbalimbali katika harakati ya kuleta maridhiano na uwiono katika eneo hilo.
Gavana Sang alisema kuwa wale wanaochochea vita katika maeneo hayo wanajulikana akitoa wito kwa asasi husika kuwataja peupe na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria, akibaini kuwa huenda wakaazi wa maeneo hayo wakakosa kupata amani kama wanaowachochea hawajachukuliwa hatua