miundomsingi duni

Wizara ya elimu katika kaunti ya Elgeyo- Marakwet ina siku 14 kufika mbele ya kamati ya elimu katika bunge la kaunti hiyo kujibu maswala yanayohusiana na  miundomsingi usioafikia mahitaji hasa ya  ujenzi wa madarasa ya shule za chekechea.

Akiongea katika bunge hilo  mweneyekiti kwenye kamati hiyo Christopher Cheboiboch alisema kuwa  kufuatia hatua za kamati hiyo za kuzuru shule tofauti imebainika kwamba baadhi ya shughuli za ujenzi wa madarasa hazikutekelezwa ipasavyo.

Mwakilishi wa wadi ya Kapsowar Joshua Kipruto alitaja kuwa ripoti hiyo imebaini changamoto watambua kamati hiyo wakifanya uangalizi wa miradi hizo na kuungwa mkono na mwakilishi mteule Peris Kiptoo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *