Wito umetolewa kwa mashemasi kuwa mstari wa mbele kuwaongoza waumini katika njia iliyosalama na inayostahili katika kufikia ufalme wa mbingu.
Akiohubiri wakati wa kupandishwa daraja kwa mashemasi katika kanisa la St.Padre Pio Friary Karen Nairobi askofu wa jimbo katoliki la Garisa George Muthaka amesisitiza haja ya mashemasi hao kuwa karibu na wanajamii ndipo wafahamu vyema maswala wanayoyapitia katika maisha yao na kuweza kuwa pamoja nao kwa njia zote na kuwaimarishia imani yao katika kristu.
Vilevile,askofu Muthaka amesisistiza haja ya mashemasi hao kujisadaka bila ya kujibakisha katika kulieneza neno lake mwenyezi mungu kila wakati hata wanapopitia changamoto maishani mwao.
Askofu huyo vilevile aliwashauri wakristu kumkaribisha mwenyezi mungu maishani mwao na kuwa tayari kutembea naye katika maisha yao kwa kumpa nafasi kubwa katika maisha yao ndipo waweze kujiweka salama katika uridhi wa mbinguni.