TULINDE CHEMICHEMI YA MAJI

Mkurugenzi wa kampuni ya kusambaza maji katika kaunti ya Uasin Gishu Peter Biwot amesema ipo haja ya mashirika na washikadau mbalimbali pamoja na wenyeji kuungana mikono katika kulinda chemichemi ya maji ili kulinda maswala ya uhaba wa maji miaka zijazo.

Akiongea katika eneo la Chebara ,afisa huyo alisema kwamba kutokana na ukatiji wa miti ovyo,imechangia pakubwa kaunti kukosa maji zaidi ya lita millioni ishirini kila mwaka na kwa hili akasema sharti wenyeji wapewe mafunzo ya kutosha kuhusiana na umuhimu wa wao kuhusika kikamilifu katika utunzaji wa chemichemi.

Aliwataka wenyeji kuwa na hulka ya kupanda miti wanapopanda angalau iwaweke salama wakaazi wote hata wakati wa kiangazi kusishuhudiwe ukame ikizingatiwa kwamba kaunti hiyom inategemea maji kwa shughuli zake mbalimbali iwe ya ukulima au matumizi ya nyumbani.

Biwot hata hivyo alisema kwamba ili kupunguza au hata kukomesha magonjwa yanayotokana na maji chafu,wenyeji wanastahili kulinda mazingira dhidi ya uchafuzi ndipo wakaazi wasije wakaugua maradhi kama vile kipindupindu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *