VIJANA WAPIGWA JEKI KUINET

Vijana katika wadi ya kuinet kapsuswa wametakiwa kubuni nafasi za ajira na kujiendeleza kimaarifa kama njia moja ya kukabiliana na umaskini na matumizi ya dawa za kulevya.

Akiongea katika warsha iliyowaletea pamoja vijana kutoka katika wadi ya kuinet Kapsuswa mwalikilshi wa wadi hiyo Rebeca Magut, amesema kuwa kuwa lengo la warsha hiyo ni kuwahamasisha vijana kuhusu namna ya kujiongezea maarifa na kubuni nafasi ya ajira, akisema kuwa hatua hiyo kadhalika inaazimia kupambana na matumizi ya dawa za kulevya ambayo kwa sasa imesakama vijana wengi kote nchini.

Amesema kuwa baada ya warsha kadhaa sawia na hiyo ambayo anapania kuandaa hivi karibuni itwapa vijana maarifa mengi ambayo itawasaidia kujikimu kimaisha na pia kuajiri wengime ikizingatiwa kuwa kwa sasa nafasi ya ajira imesalia kuwa kitendawili.

Naye mkurugenzi kutoka katika idara ya vijana kaunti hii ya Uasin gishu Peter Ruto amesema kuwa serikali ya kaunti ya Uasin gishu iko mbioni kuwapiga jeki vijana ili kupata namna ya kujiajiri kupitia kwa vikundi mbalimbali, hii ikiwa mojawapo ya mikakati ya serikali kupunguza visa vya uhalifu na utovu wa usalama katika kaunti hii ya Uasin gishu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *