maridhiano kupitia mazungumzo

Viongozi wa kidini katika kaunti ya Uasin Gishu wameendelea kuwaomba viongozi wa kisiasa kuhakikisha matamshi yao hayachochei uhasama miongoni mwa wakenya.

Wakiongozwa na Sheikh Abubakar Bini na Kasisi Paul Mburu,viongozi hao walisema kwamba amani itaafikiwa tu iwapo wanasiasa watajitenga na matamshi ya uchochezi wanapowasuta wenzao wasiowaunga mkono kwa hili wakisema kwamba amani itapatikana na maridhiano.

Wakati huo,viongozi hao walisisitiza haja ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuruhusu fursa ya mazungumzo baina yake na serikali ili matakwa yake aliyoyatoa na kama upane wa Azimio ziweze kushughulikiwa,wakimtaka Odinga kutokuwa mtu asiyeeleweka kwani wanasema anastahili kuamua iwapo anahitaji mazungumzo yafanyika au wasitishe ndipo muda mwingi usipotee kwa kurudia maswala ambayo yangetatuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *