Kumbatieni mwito wa amani kwa manufaa ya wote

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amewataka wenyeji katika eneo la Kerio Valley kujitenga na maswala yasiyokuwa na mwelekeo katika maisha na kuhakikisha kwamba wamekumbatia mwito wa amani.

Akiongea afisini mwake mjini Eldoret,askofu Kimengich alisema kwamba wakaazi eneo hilo wanastahili kukubali kufanya mazungumzo na wanaozozana nao ili mwafaka upatikane.

Alitaja utamaduni wa wizi wa mifugo ndipo vijana kuweza kutoa poza kwamba umepitwa na wakati na wanapaswa kuweka maanani mbinu ya kujiinua kimaisha iwe kupitia kuungana mikono katika vikundi mbalimbali vya biashara ama hata kuwapeleka wanao shuleni ndipo waweze kuwa na mtazamo tofauti katika maisha na yenye kuwajenga katika maisha yao siku za hapo baadae

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *