Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga mchana wa leo anaongoza mkutano wa BBI kwenye kaunti ya narok.
Mkutano huo umeandaliwa ili kuweza kuangazia kwa undani changamoto ambazo zinakuwa zikiwakumba wenyeji waeneo hilo na kujumuishwa kwenye ripoti ya mwisho ya BBI.
Swala la ardhi na dhulma za kihistoria zinatarajiwa kusheheni hotuba ya viongozi wa jamii ya maa hii leo kwenye mkutano utakaoandaliwa mjini Narok kujadili ripoti ya BBI. Wajumbe waliozungumza hio jana kwenye kikao mjini humo wamedai haki kutokana na dhuluma za kihistoria, wakikariri kuwa ni sharti mashamba yao kulindwa na haki za rasilimali zinazopatikana eneo hilo kusaidia jamii ya wamaasai.