KMPDU YALIMA SERIKALI GATUZI

Muungano wa madaktari,wauguzi na matabibu kanda la kaskazini mwa Bonde la ufa KMPDU Umeipa serikali za  gatuzi eneo hilo ilani ya mgomo iwapo serikali hizo hazitatekeleza makubaliano yaliyotiwa saini kwenye mkataba ya maelewano ya CBA.

Wakiongea hapa  mjini Eldoret wakiongozwa na katibu wao tawi la North Rift Mulei Makonzi, muungano huo umesikitishwa na uongozi wa serikali hizo kwa kile unadai kuwa gatuzi hizo zimedinda kutekeleza makubaliano hayo ambayo yalependekeza kuwa wahudumu wa afya ukanda huo wapandishwe vyeo au daraja pamoja na kuongezewa mshahara.

Wahudumu hao vilevile wameapa kutoandaa  mkutano mwingine wa mazungumzo wakisema kwamba sharti matakwa ya wahudumu hao yashughulikiwe.

Yanajiri haya wakati na ambapo wahudumu nchini mnamo Januari mwaka huu walitishia kuingia kwenye mgomo kwa kigezo kwamba serikali ilikosa kutekeleza makubaliano baina yao licha ya makubaliano yaliyotiwa sahihi kati yao na serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *