NJIA YA AMANI NI MAZUNGUMZO

Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini chini ya uenyekiti wake askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Mombasa Martin Kivuva Musonde limetoa wito kwa viongozi hao wawili ambao ni Rais William Ruto na Raila Odinga kulegeza misimamo yao na kuandaa mdahalo kwa faida ya mshikamano wa kitaifa.

Askofu mkuu Kivuva amemtaka kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga kusitisha maandamano hayo kwa kuwa wakristu wanaanza  juma takatifu huku wenzao waislamu wakiendelea na mfungo wa Ramadhani wakati ambapo wakenya wanahitaji utulivi na kuzungumza na mwenyezi Mungu.

Naye askofu wa kanisa la ACK Paul Korir ametoa wito kwa serikali ya Kenya kwanza kukoma kujipiga na kulegeza misimamo yao na ili kuwaita wenzao wa Azimio kwenye meza ya mazungumzo, akisema kuwa ni mazungumzo tu ndiyo yatakayorejesha taifa hili katika hali ya utulivu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *