wafanyikazi hewa matatani

Serikali ya kaunti ya uasin gishu hivi karibuni itaanza machakato wa kuwafanyia wafanyikazi wa kaunti hiyo ukaguzi ili kuwatambua na kuwaondoa wafanyikazi hewa.

Katika kikao na wanahabari gavana wa kaunti hii ya Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim amesema kuwa wafanyikazi hewa ni wengi katika kaunti wengi wao wakiwa wale waliostaafu ilhali bado wanapokea mishahara, wengine wakiwa ni wale kwa vyovyote vile hawafanyi yoyote katika kaunti, jambo ambalo gavana Chelilim anasema kuwa inalemaza miradi mingi ya maendeleo kwenye kaunti hiyo.

Gavana Chelilim amesema kuwa mchakato huo utaendeshwa kwa utaratibu na kwa mujibu wa sheria ili kuwaondoa wafanyikazi hewa, zoezi ambalo anasema litang’oa nanga hivi karibuni. Hata hivyo ametoa wito kwa vijana kujifunza hulka ya kuweka akiba kwa manufaa yao siku za usoni akisema kuwa wengi wa wale wanaostaafu katika nyadhifa mbalimbali wanasalia katika lindi la umaskini kutokana na ukosefu wa akiba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *