MTOZA USHURU MPYA UASIN GISHU

Serikali ya kaunti ya Uasin Gishu inapania kukusanya zaidi ya shilingi milioni mia nne katika kipindi cha majuma mawili yajayo, hii ni kufuatia jopo kazi ambalo limebuniwa na gavana wa kaunti hiyo Jonathan Bii chelilim ili kufankisha zoezi la ukusanyaji ushuru.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa jopo hilo Gavana Jonathan Bii Chelilim amesema kuwa lengo kuu la kubuniwa kwa jopo hilo, ni  kuhakikisha kuwa kila mfanyibiashara kwenye kaunti anapata fursa rahisi ya kulipa ushuru kinyume na chanagmoto ambazo zimeshuhudiwa hapo awali zikiwemo hata ukwepaji wa kulipa ushuru.

Gavana huyo amewahakikishia wafanyibiashara na wale wanaopania kuwekeza kwenye kaunti hiyo kuwa serikali yake itaweka mazingira bora ya kufanya biashara, akihoji kuwa tafiti ambazo zimefanywa hivi karibuni zimeweka kaunti hii katika ramani nzuri akitoa wito kwa kila mkaazi na mfanyibiashara kusaidia katika shughuli za kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kulipa ushuru.

Amesema kuwa zoezi hilo kadhalika litasaidia katika machakato wa kubuni nafasi za ajira kwa vijana ambao kwa sasa wanakumbana na jinamizi la ukosefu wa ajira jambo ambalo anasema imepelekea vijana wengi kukwama kwenye lindi la umaskini na wengine kujiingiza katika visa vya uhalifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *