Mbunge mteule wa chama cha United Democratic Alliance Joseph Wainaina ameitaka upande wa upinzani kuyakubali matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita na kufuata sheria kwa kuikosoa serikali kwa mujibu wa katiba.
Akiongea mjini Eldoret,Wainaina alisema kwamba msimu wa siasa ulikwisha nan i fursa ya serikali iliyo madarakani kuwafanyia wenyeji kazi na sio kila kuchao kuendeleza siasa na vitisho vya maandamano.
Alisema kwamba katiba inawaruhusu kuikosoa serikali ila ni kwa njia inayostahili na kuwataka kukoma kuwarudisha wakenya nyuma ilhali wao wanasubiri maendeleo.