Hali tete Kerio Valley

Viongozi kutoka ukanda wa Northrift sasa wanamtaka waziri wa usalama wa ndani profesa Kithure Kindiki kuweka mikakati maalum ya kukomesha mauaji katika eneo la Bonde la Kerio la sivyo ang’atuke mamlakani.

Wakiongozwa na seneta wa kaunti ya Elgeiyo marakwet William Kisang viongozi hao wamesema kuwa maafisa wa jeshi la KDF waliotumwa kulinda doria katika eneo hilo, bado hawajaanza kutekeleza operesheni wakisema kuwa kwa sasa operesheni inaendelezwa na maafisa wa polisi wala sio KDF, jambo wanalosema limepelekea wengi kupoteza maisha yao katika maeneo tofauti kwenye bonde la Kerio.

Mbunge wa Keiyo Kusini Gideon Kimaiyo almaarufu Sonko ametoa wito kwa rais Wiliam Ruto  kushinikiza waziri huyo wa usalama kukomesha visa vya mauaji, la sivyo apigwe kalamu, kauli sawia na hiyo kadhalika imetolewa na mbunge wa Kesses Julius Ruto ambaye ametoa wito kwa waziri Kindiki kutuma notisi ya kuwaruhusu wanajeshi kutekeleza operesheni hiyo  bungeni haraka iwezekanavyo, ili kuidhinishwa na wabunge kama hatua ya kuwaruhusu wanajeshi hao kutekeleza operesheni bila kuongozwa na maafisa wa polisi.

Nawe mbunge wa Mosop Abraham Kirwa ametoa wito kwa idara ya ujasusi kuwachukulia hatua kali na kuwaadhibu wanasiasa na viongozi mashuhuri ambao wanasemekana kuwa ndio wanafadhili uhalifu katika maeno hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *