Askofu msimamizi wa makanisa ya Apostlic Churches Eldoret Mugo Njenga ameitaka jopo kazi inayosimamia shughuli ya kuwapiga msasa majaji ambao wanapaswa kuchukua nafasi katika mahakama za humu nchini kwamba, waweze kuwapa nafasi majaji ambao watasimama kidete na kufuata sheria za taifa hili ila sio kwa wale walio na ubinafsi.
Akiongea na wanahabari mjini Eldoret,askofu Mugo alisema uongozi wa mahakama unahitaji watu wenye msimamo dhabiti na sio wale ambao ni wafisadi ndipo wenyeji waweze kupata haki kila muda.
Alitumia fursa hiyo kuikemea vikali uamuzi wa mahakama upeo ya kuwapa uhuru vikundi vya wasagaji,mashoga na watu walio na mahusiano ya jinsia moja akisema inaenda kinyume na maadili na mafundisho ya bibilia.
Askofu huyo aliwataka walimu na hata jamii kwa jumla kuchukua jukumu lake la kuwaelimisha watoto wakiwa wadogo hasa kuhusiana na athari za hulka hizo kwa hili akieleza itasadia pakubwa tabia na mienendo ya watoto kuwa imara hata wanapokubwa na msukosuko wa aina yoyote.