Wizara ya madini nchini imeahidi kuifufua tena kampuni ya Flouspar katika kaunti ndogo ya Keiyo Kusini katika kaunti ya Elgeyo-Marakwet ili kuweka hai matumaini ya wakaazi eneo hilo.
Akiongea baada ya kuzuru eneo eneo la Sugutek waziri wa madini Salim Mvurya ameweka bayana kwamba wenyeji watafurahia uwepo wa kampuni hiyo kwa mara nyingine tena baada ya kufungwa mwaka wa 2016 kwani itawapa wengi wa vijana nafasi za kazi pindi itakapofufuliwa.
Kwa upande wao wakazi wa eneo hilo waliitaka serikali kuhakikisha waliokuwa wametoa kipande cha ardhi wamefidiwa ndipo waweze kufurahia uwepo wa kampuni hiyo.