Kumbatieni maridhiano

Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Subira Anyolo ametoa wito kwa wanasiasa kusitisha mikutano yanayoendelea nchini kwa sasa na badala yake wakumbatie maridhiano kwa manufaa ya mshikamano wa kitaifa.

Akizungumza katika hafla ya kuzindua rasmi kampeni ya kwaresima ambayo imejikita katika nguzo tatu muhimu ambayo ni toba, sala na kuwasaidia wasiojiweza askofu mkuu Anyolo amesema kuwa joto la kisiasa nchini linaathiri shughuli nyingi za maendeleo akiwataka wanasiasa kutumia mbinu mbadala ya kutatua tofauti zao.

Askofu kadhalika aliwataka wakristu na waumini wote kwa jumla kusuluhisha tofauti zao akisema kuwa ukosefu wa kuluhisha migogoro kwa wakati ufaao ndio huleta uhasama kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *