Ulimwengu unapoadhimisha siku ya saratani ,wito umetolewa kwa wananchi kujua hali yao ya kiafya mapema ndipo waweze kupokea matibabu na kuepuka maafa yanayotokana na ugonjwa huo.
Akiongea katika hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi Eldoret MTRH,mkurugenzi wa hospitali hiyo Wilson Arwasa ni kwamba vifo vingi vinavyosababishwa na saratani hutokana na mgonjwa kujua hali yake ikiwa katika kitengo cha mwisho ambacho kwa asilimia kubwa ni ngumu kutibika hivyo kuwataka wananchi kuwa mstari wa mbele kujipima akisema kuwa kila muda hospitali hutoa huduma hizo bila malipo yoyote.
Aliwashauri wakazi kuwa waangalifu na jinsi wanavyoishi na vyakula wanavyokula kwa sababu ndizo vyanzo vikuu vya saratani.
Kadhalika,Arwasa alidokeza kwamba wanaendelea na hamasisho la umma kuhusiana na athari za ugonjwa huo,na jinsi wanavyoweza kuendelea vyema na maisha yao hata baada ya kuwa waathiriwa na maradhi hayo.