Viongozi wa kidiniĀ sasa walijitokeza kulaani visa vya uhusiano wa kimapenzi ya jinsia moja wakisema kuwa ni hulka ambazo ni kinyume na maandiko kwenye bibilia.
Wa hivi punde ni mwenyekiti wa maimamu kaskazini mwa bonde la ufa Sheikh Abubakar Bini ambaye alitoa wito kwa jamii kamwe kutokubali hulka hii ambayo anasema kwa sasa imeanza kuenea humu nchini.
Alikashifu kisa cha hivi majuzi ambapo walimu wa shule moja kule Kisii waliwalazimisha wanafunzi kushiriki tendo linaloashiria ngono ya jinsia moja, jambo analosema huenda likawa ni shinikizo kutoka kwa wale wanaotaka kuendeleza hulka hiyo humu nchini.