Marehemu Bruda Paul alikuwa mwalimu aliyechangia pakubwa ukuaji wa Imani katika jimbo hili la Eldoret.
Ni kauli yake Padre Fredrick Njoroge akihubiri katika Misa ya wafu kwa ajili ya Bruda Paul Brendan ambapo alimkumbuka kama mtu mkarimu na mcheshi aliyewavutia wengi ambao hawakuwa Waumini wa kanisa katoliki katika Imani ya kikatoliki.
Amesema kuwa marehemu Bruda Paul alikuwa nguzo muhimu kwa kuwaleta vijana wengi kwenye kanisa kupitia talanta Yao ambaye yeye mwenyewe alikuwa anakuza.
Alisema kuwa kanisa limepoteza mtu ambaye alikuwa mwadilifu na aliyejisadaka bila kijibakisha katika utendakazi wake kama bruda.