KAMISHNA NYALE:Usalama upo fanyeni biashara kwa bidii

Kamishna wa kaunti ya Uasin Gishu Dkt.Eddyson Nyale amewahakikishia usalama wa kutosha kwa wafanyibiashara katika soko lilipolekwa eneo la Kimumu wanapoendeleza biashara zao.

Akiongea na wanahabari mjini Eldoret Nyale alisema maafisa wa usalama wameimarisha usalama meaner hayo hivyo akawataka wafanyibiashara kutohofia lolote kwani idara hiyo iko imara kwa jukumu lake.

Kadhalika alisema mipango imewekwa ya kuweka taa kwenye soko hilo akibaini kwamba biashara imeshika kazi na wananuia kuinua maisha ya wakaazi na uchumi wa nchi kupitia biashara.

Kadhalika,Nyale aliwaonya wahalifu wanaoendeleza uhalifu kwamba siku zao zimehesabiwa na kwamba wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *