Askofu mpya wa jimbo Katoliki la Kitale Henry Juma Odonya alimshukuru Mungu kwa uteuzi wake huku pia akimshukuru msimikaji wake askofu mkuu Herbatus Matheus Maria van Megen kwa ushauri, wosia na kazi yake nzuri.
Wakati uo huo askofu Juma alimsifia mtangulizi wake askofu Maurice mstaafu Maurice Antony Crowley kwa kazi yake nzuri hasa hatua zilizopigwa katika kuchochea miito mitakatifu jimboni, kuimarisha sekta ya elimu na huduma kwa jamii.
Vilevile aliwshukuru wazazi wake, ndugu jamaa na viongozi wa kanisa wakiwemo maaskofu, mapadre, watawa na makundi mbalimbali ambao amewataja kuwa nguzo kuu katika kufikia daraja la uaskofu.