Hisia mseto zinazidi kuibuliwa na wakaazi wa kaunti hii ya Uasin gishu baada serikali kupitia wizara ya elimu kupendekeza kuwa wanafunzi watakaojiunga na shule za sekondari za msingi kuwa na sare tofauti na ile waliokuwa wakitumia hapo awali katika gredi ya sita.
Waziri wa elimu Ezakiel Machogu alisema kuwa licha ya wanafunzi hao kusalia katika shule zao za hapo awali, bodi ya usumamizi wa shule pamoja na wazazi wataandaa kikao ili kutathmini sare tofauti na ile waliotumia katika gredi ya sita kwa wale watakaojiunga na shule za sekondari za msingi.
Waziri huyo alikariri kuwa sare hizo zitagharamiwa na wazazi, swala ambalo limezua hisia kinzani miongoni mwa wakaazi wa kauni hii, wakitoa wito kwa serikali kuingilia kati wakisema kuwa hali ilivyo kwa sasa kuichumi huenda ikawasakama wazazi.
Baadhi ya wazazi kadhalika wakidai kuwa watakadiria hasara kuwa kuwa tayari walikwisha wanunulia wanao sare na kule kubadilisha sare itawapelekea kugharamika kwa maradufu wengine wakidai kuwa hali hiyo ni ya kawaida kwa kuwa kila wakati wazazi hulazimika kuwanunulia wanao sare kila wakati shule zinapofunguliwa,