ASKOFU ANYOLO:Kristu awe kiongozi wenu maishani

Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Anyolo aliwashauri wakristu kumkaribisha kristu kwa kujitolea kumtumikia mungu kupitia msaada wao kwa wengine.

Akihubiri wakati wa misa ya kipaimara katika kanisa la Mtakatifu Matia Mulumba Thika amesema kwamba ukristu udhihirika kupitia kwa wao kujitolea na kuwa msaada wa wengine bila ya majigambo.

Aliwahimiza wakristu kuishi maisha ya haki kwa kuzingatia mwongozo wa maisha yaliyo safi na kuwa watu ambao wanaweza wakaigwa katika jamii.

Aliwataka kujiepusha na maswala ambayo huenda ikawaresha nyuma ikiwa ni pamoja na wivu na masengenyo akieleza kwamba maisha yaliyobora ni kuwa mkristu mtimilifu na mwenye huruma kwa wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *