Askofu anayestaafu wa jimbo katoliki la Kitale Anthony Maurice Crowley amewapongeza wote waliomuunga mkono wakati wa kuhudumu kwake kama askofu kwa kile amesema amefurahia matunda ya uongozi wake kwani amekuza miito kadhaa za mapadre.
Akiongea katika shule ya Mother of Apostle Seminary Eldoret wakati wa ibada ya shukrani kwa kuhudumu kwake,ammebaini kwamba japo alishuhudia changamoto si haba wakati akiwa akiongoza taifa la bwana,anafurahia sana hatua ambayo aliweza kupiga kwa kuwainua wengine kutimiza ndoto zao za kuhudumu katika shamba la bwana.
Wakati huo,askofu Crowley aliwapongeza wakristu na kila mmoja alichangia utendakazi wake unakwenda vyema japo anasema changamoto zipo ila aliweza akazikabili na kusimama kidete katika kuwasaidia wengine kupata kumjua na kufuata yesu kristu.
Kadhalika,aliwasihi mapadre wapya na watumishi wote katika shamba la bwana kuwa wenye huruma,upendo na kuweka sala kipaumbele ndipo waweze wakaongoza vyema wakristu katika safari ya mbingu.
Askofu Anthony Maurice Crowley aliweza kuhudumu katika dyosisi ya Eldoret alipokuwa kasisi kabla ya kuzimikwa kuwa askofu wa jimbo katoliki la Kitale wakati huo pia akahudumu kama askofu msimamizi wa dyosisi ya Eldoret wakati askofu wa Jimbo la Eldoret Marehemu Cornelius Korir alipoaga dunia kabla ya kuyavua viatu hivyo pindi askofu wa sasa Dominic Kimengich kuchukua usukani kama askofu wa Eldoret.