Makanisa watoa msaada kwa waathiriwa wa baa la njaa

Wakenya wakiendelea kusherehekea siku kuu ya krismasi viongozi wa kidini kutoka katika kaunti hii ya Uasin Gishu kwa ushirikiano na serikali ya kaunti wametoa msaada wa chakula kwa wakaazi wanaokumbwa na baa la njaa.

Viongozi hao chini ya vuguvugu ya save a life ambayo iliasisiwa na gavana wa kaunti hii ya Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim, wametumia shamrashamra za krismasi kukusanya msaada kutoka kwa waumini walio na mapenzi mema kwa lengo la kuwapelea wakaazi ambao wanakumbwa na baa la njaa haswa katika eneo la Mrigat kaunti ya Baringo.

Waziri wa barabara na uchukuzi katika kaunti hii ya Uasingishu mhandisi Joseph Lagat akizungumza katika afisi za kaunti hiyo amewapongeza viongozi hao wa makanisa kwa kujitolea kupiga jeki vuguvugu hiyo na halkadhalika kuwa na nia ya kuwasaidia wake ya ambao kwa sasa wanakabiliwa na makali ya baa la njaa.

Kwa upande wao viongozi hao wa kidini wakiongozwa na kasisi Peter Gatiru amesema kuwa wamefanikiwa kupata gunia thelathini na tano  ya chakula kwa lengo la kupiga jeki vuguvugu hiyo.

Haya yanajiri wiki mbili tu baada ya gavana Jonathan Chelilim kuzindua vuguvuvugu hiyo ambayo ilipelekea familia zaidi ya elfu tano kunufaika na misaada hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *