Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amemtaka rais William Ruto kukaza kamba katika juhudi za kuwatumikia wakenya kwa kutekeleza ahadi alizotoa wakati wa kampeni, na hata kuwahudumia wale waliomchagua na wale hawakumchagua.
Akiongea katika eneo la Sports Club Eldoret wakati wa maombi ya Shukrani, askofu Kimengich amerai rais kuwa maslahi ya wenyeji ni la kuangaziwa ili wenyeji waweze kuhisi uwepo wa uongozi wa kitaifa na kujituma kuinua uchumi wa taifa hili.
Amewataka viongozi wa kisiasa kuweka siasa kando na badala yake kuwahudimia wakenya na kadahalaika kutekeleza ahadi walizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka wa 2022 kwa usawa bila kuangalia miegemeo ya kisiasa.
Wakati hupo amewashauri wenyeji kuwa mstari wa mbele kuilinda taifa hili kwa kujikakamua kazini na kuipenda nchi hii kwa faida ya mshikamano wa kitaifa.
Aidha,Askofu Kimengich amewaomba wakenya kuwa na huruma kwa wale ambao hawana uwezo wa aina yoyote katika jamii iwe ya chakula,mavazi au hata kulihubiri neno lake kristu kwao kwa kuwapa matumaini katika maisha.
