Sharti makamishna wangatuliwe

baadhi ya wabunge eneo la bonde la ufa wakiongozwa  na mbunge maalum wa  chama cha UDA Joseph Wainaina  wameapa kuwa  sharti makamishna wanne wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini ya IEBC  waondolewe afisini licha ya  tishio za  mandamano kutoka kwa mrengo wa upinzani.

Akiongea mjini Eldoret,Wainaina alisema kwamba  licha ya upizani kuahirisha mandamano yaliyoratibiwa kati  miji ya mikuu ya Nairobi , Nakuru , Mombasa na mji wa Kakamega hadi  mwezi ujao, serikali   haitaruhusu  kuwepo mandamano hayo  na  wala bunge halitashawishika kutopitisha  kubuniwa tume ya kuchunguza na kupendekeza kuondolewa makamishna hao.

Alidokeza wanne hao wakiongozwa na naibu mwenyekiti wa IEBC Juliana Cherera na wenzake  ambao  hawakuafikiana na mwenyekiti wa  tume hiyo  Wafula Chebukati kuhusiana na matokeo ya  uchaguzi mkuu wa  mwaka 2022 Sharti wangatuliwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *