TRANSPARENCY INT’L LAKUTANA NA WANASIASA

Maswala ambazo zimeibuka baada ya mkutano wa siku tatu kati ya viongozi wa kisiasa wanaowania nyadhifa mbalimbali katika kaunti ya Uasin Gishu na shirika la Transparency International ni kwamba wakenya wengi wanamatumaini makubwa kutoka kwa viongozi hao kuhangazia maendeleo na kulinda mali ya umma.


kwa mujibu wa afisa kutoka shirika la Transparency International tawi la Uasin Gishu Alex Yator ni kwamba kutokana na mkutano huo uliowaleta pamoja washikadau mbalimbali pamoja na wakaazi ,imabainika kwamba swala la ufujaji wa mali za umma umekua donda ndugu na wakaazi wakiwataka viongozi watakaochaguliwa kwenye uchaguzi mkuu ujao waweze kuwajibikia utendakazi wao bila ya kulaghai wakenya pesa za maendeleo mashinanai.

Hata hivyo,afisa huyo aliwataka wenyeji kuungana mkono ndipo amani iweze kudumishwa taifa linapojiandaa kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *