CJPC ELDORET: KAFYU IMEZAA MATUNDA KERIO

Mratibu katika afisi ya haki na amani katika jimbo katoliki la Eldoret Samwel Kosgey amesema hatua ya kuwekwa kwa kafyu imezaa matunda katika kuimarishwa kwa amani katika bonde la Kerio.

Akiongea mjini Eldoret,Kosgey alisema amri ya kutotoka nje imechangia sana usalama wa wakaazi na kwa hili akipongeza hatua hiyo.

Vilelvile,afisa huyo aliwataka wenyeji maeneo hayo kuendelea kudumisha amani na kuwashauri vijana ambao huenda wanatumika vibaya kuzua rabsha maeneo hayo kujitenga na shughuli hizo ambazo ametaja hazina mwelekeo wowote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *