Kamishna;MTAPATA KUFIDIWA

Kamishna wa kaunti ya Uasin Gishu Stephen Kihara amewahikikishia wakaazi maeneo ambayo barabara mbadala [By pass] unapita hasa maeneo ya Cheptiret-Kapseret kwamba watapata kufidiwa kwa muda unaofaa.

Akiongea mjini Eldoret Kihara alidokeza kwamba yapo baadhi ya vigezo ambavyo vilichangia kucheleweshwa kulipwa kwao ikiwemo mzozo wa familia ambazo zilikuwa zifidiwe.

Kamishna huyo vilevile alisema kwamba idara ya usalama ikishirikiana na mamlaka ya barabara nchini Kenha Itawafidia wenyeji wote waliotoa ardhi yao kwa ujenzi wa mradi huo kwa muda mwafaka waliokuwa wameagana bila ya kuwapitisha muda akiwaomba wenyeji hao kuwa na subra.

Kadhalika alisema shillingi billioni 4 imetengwa kwa ajili ya ufadhili huo na hivyo akawataka wakaazi hao kutohofu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *