Parokia ya moyo mtakatifu wa Yesu kathdrali limesherehekea siku ya familia siku ya Jumapili.
Akihubiri katika Misa hiyo askofu Dominic Kimengich alisema kuwa amtegemeae kristu atapata kimbilio, Baraka na usalama pamoja na huruma wa bwana
Askofu amesifia kujitolea kwa wakristo wa parokia hiyo kufanikisha kanisa Hilo kwa kuweka sanamu ya Yesu langoni mwa kanisa Hilo ambayo ni dhihirisha ya imani dhabiti akiwapongeza kwa kulikarabati jumba la kuabudiwa kwa ekaristia takatifu.
Alitoa wito kwa wakristo kuwa na kiu ya kupokea ekaristia takatifu Kila wakati na kushiriki Toba Kila mara.
Kadhalika aliwapongeza wakatekumeni waliopokea sakaramenti ya kipaimara hii Leo.
