AFUENI KWA WAKULIMA WA KAHAWA TRANS NZOIA

Serikali imelazimika kuingilia kati kusuluhisha mzozo wa uongozi wa shirika la kijamii la ukuzaji kahawa la Kiungani Growers Co-operative Society katika kaunti ya Trans-Nzoia ambao umedumu kwa ya mwongo mmoja sasa na kutishia kulisambaratisha.

Sammy Laraboru ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa shirika hilo anasema uongozi wa shirika hilo umekuwa wa kiimla ba kufanya maamuzi pasi na kuwahusisha wanachama.

Wanachama wa shirika hilo sasa wanamtaka waziri wa kilimo Peter Munya kufanya kipaumbele ukuzaji wa mikahawa sawa na alivyofanya katika sekta ya majani chai.

Naibu kamishna wa tarafa ya Kiminini Mogere Lumumba ameagiza uongozi wa sasa kutofanya mikutano yeyote kwa kipindi cha mwezi mmoja ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *