KERO YA VIWAVI JESHI

Wakulima wa mahindi katika eneo la Moiben kaunti ya Uasin Gishu wameelezea hofu ya kupata mavuno duni ya mimea yao kufuatia uvamizi wa viwavi jeshi katika eneo hilo kwa muda wa majuma mawili sasa

Wakulima hao wanasema kwamba wametumia rasilimali nyingi kwa shughuli za upanzi hali ambayo pia imechangiwa pakubwa na kupanda kwa bei ya mafuta.

Baadhi wanasema walichukua mikopo kununua mbegu, mbolea na vifaa vingine vya kilimo na wanahofia itakuwa vigumu kulipia mikopo yao ikiwa wadudu hao waharibifu hawatadhibitiwa upesi.

Wakizungumza katika eneo la Moiben wakulima hao sasa wanaitaka serikali za kaunti na wizara ya kilimo kuingilia kati ili kuwaepushia hasara zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *