Askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Eldoret Yohane Kiplimo Lelei ametilia shaka hatua wale waliokamatwa hapo jana wakuhusishwa na mauji ya paroko wa parokia ya St Matia Mulumba Tot.
katika kikao na wanahabari askofu Lelei amesema kuwa wale waliohusika na mauaji hayo wanajulikana katika eneo hilo ilhali maafisa wa usalama wamedinda kuwakamata, na kwamba wenyeji wa eneo hilo wanawafahamu kwa kina wale waliohusika, akipuuzilia mbali madai kuwa watu sita waliokamatwa ndio walikuwa wahusika wakuu wa mauaji hayo.
askofu Lelei kadhalika amemtaja padre Bett Kama mtu aliyejisadaka bila kujibakisha katika kazi yake ya kitume akinyoshea kidole cha lawama maafisa wa usalama ambao walihoji kuwa kisa cha mauaji hayo hayahusishwi na wizi wa mifugo na kutoa wito kwao kufanya uchunguzi wa kina na kuwakamata wahusika wakuu.
