Kituo maalum cha kuwapa hifadhi waathiriwa wa dhuluma za kijinsia maarufu cha Hope Recovery kimezinduliwa rasmi katika kaunti ya Elgeyo Marakwet.
Kulingana na afisa anayesimamia idara ya kuzuia dhuluma za kijinsia katika kaunti hiyo Philemon Kittony, visa 100 za dhuluma za kijinsia vimerepotiwa katika kaunti hiyo Kwa miezi 3 zilizopita
Kwa upande wake afisa kutoka shirika linalookoa waathiriwa wa dhuluma za kijinsia maarufu kama Gender Violence Recovery Center Elizabeth Atwani, amesisitiza umuhimu wa kituo hicho akisema kuwa itakuwa afueni kwa waathiriwa wa dhuluma za kijinsia katika kaunti ya Elgeyo marakwet