Wito umetolewa kwa wakristu kuhakikisha kwamba wanaheshimu kauli ya wnegine kwa kuwa kila mwanadamu anamtazamo tofauti katika maisha.
Balozi wa baba Mtakatifu Nchini Herburtus Maria Van Megen amesisitiza kuwa kila mmoja ananafasi ya kujieleza na ni vyema kusikilizwa ijapokuwa kauli zao sio za kumpa mwenzake kukata kauli.
Amesema kuwa ulimwengu wa sasa unapaswa kuwa wa kuelewana ili watu wapate kusaidiana na kupanua mawazo yao.
Kadhalika,balozi Van Megen amewataka wakristu kujivunia ukristu wao maana ndio njia pekee ya kuwaweka mbele kiimani na kuwasaidia kujikatia tiketi kuridhi ufalme wa mbingu.