Wito umetolewa kwa watu katika jamii kuhakikisha wanashirikiana ili kukabiliana na jinamizi la ukatili wa jinsia ambao unashuhudiwa kwa sasa katika jamii.
Akizungumza katika chuo kikuu cha Tangaza jijini Nairobi,askofu wa Maralal Hieronimus Emusugut Joya amesikitikia visa vingi vya dhulma za kijinsia zinazoshuhudiwa nchini akisema sharti suluhu la kudumu kuwepo.
Alisema kwamba yastahili kwa watu kuwa na uhisiano mwema na kutafuta njia mbadala ya kutatua tofauti zao, tofauti na kutumia nguvu au hata kuwaumiza wengine wanapotaka haki.