Embu yafanikiwa mchungaji mwingine

Monsinyori Peter Kimani Ndungu’ ametoa wito kwa wakristu wa jimbo la Embu kumuombea anapojiandaa kupata Daraja la uaskofu.

Katika kikao na makleri na majando kasisi wa jimbo Hilo saa chache tu baada ya kuteuliwa na baba mtakatifu kuwa askofu wa nne wa jimbo katoliki la Embu Monsinyori Peter Kimani ametoa wito kwa wakristu wa jimbo Hilo kumpa motisha kupitia Sala na ushirikiano ili aweze kuliongoza jimbo Hilo kwa mchungaji wa nne wa jimbo Hilo.

baba mtakatifu alimteua Padre Peter Kimani na askofu msaidizi wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Wallace Nganga kuongoza jimbo la Embu na jimbo la jeshi mtawalia.

Ikumbukwe kuwa jimbo la Embu limekuwa chini usimamizi wa askofu mkuu Anthony Muheria baada askofu wa jimbo Hilo karuiki njiru kuteuliwa na baba mtakatifu Francisko kwenda kulianzisha jimbo jipya la Wote.

monsinyori Peter Kimani atakuwa wa kwanza baada mwadhama John kadinali Njue kuwa askofu wa kwanza akifuatwa na askofu Anthony Muheria na Kisha baadaye askofu Paul Kariuki Njiru kama askofu wa tatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *