Gavana wa kaunti ya Uasin Gichu Jonathan Bii Chelilim amesema serikali kupitia wizara ya barabara na uchukuzi kaunti hiyo imepiga hatua kubwa ya kuhakikisha kuwa kila kaunti ndogo imepata kuendelea na shughuli zao za kila muda kupitia kukarabatiwa kwa barabara hizo na kuwarahisishia shughuli zao za uchukuzi.
Akizungumza katika eneo la Kapseret wakati wa kuzindua shughuli hiyo,Chelilim alisema kwamba serikali imetenga pesa kwa minajili ya kuwekwa kwa alama zaidi barabarani ya zaidi ya kilomita 200 kwenye barabara za mashinani.
Amewataka wenyeji kutumia fursa hiyo kujishughulisha na biashara ndipo waweze kujikwamua kwa umaskini unaotokana na hali ngumu ya maisha.
Kwa upande wake,waziri wa barabara ,miundombinu na uchukuzi katika kaunti ya Uasin Gishu Mhandisi Joseph Lagat alisisitiza kwamba hatua hii ya ukarabati ni njia mojawapo ya kusaidia kuyaziba mihanya kwenye barabara hasa msimu wa mvua na kupunguza mafuriko barabarani.