Viongozi katika kaunti ya Uasin Gishu wamewaomba wahisani kuendelea kushirikiana na wakenya wengi kutoa msaada wa chakula ndipo wakenya wanaokabiliana na makali ya njaa wapate kufaidika.
Wakiongea mjini Eldoret wakiongozwa na kamishna wa kaunti ya Uasin Gishu Dkt.Eddyson Nyale ,gavana Jonathan Bii Chelilim na baadhi ya viongozi wa kidini wakiongozwa na Sheikh Abubakar Bini wamesema wamenedelea kupokea chakula ambpo walipokea zaidi ya magunia mia moja ya mahindi cha msaada wamewarai wenyeji kujitokeza na kuungana mikono kukabiliana na baa la njaa.
Wamewataka wenyeji kutowasahau wenzao maana wote ni wakenya wapenda amani na wanaojali maslahi ya wengine.