YESSEN HASSAN:Vijana twapenda amani

Viongozi wa vijana wamewapongeza vijana nchini kwa kudhihirisha uweledi wao wa kuweza kudumisha ,kuhubiri na kuikuza amani msimu wa kampeni na uchaguzi uliopita wa mwaka huu kwa njia ya amani.

Kwa mujibu wa msimamizi wa vijana kanda la kaskazini mwa bonde la Ufa Yessen Hassan alisema msimu huo uliopita ulikuwa wa mpito kwa vijana wengi ikizingatiwa kwamba macho yote yalikuwa yameelekezwa kwa vijana kwa hulka na kasumba ya hapo awali ya kuzua vurugu ila kwa sasa akisema vijana hao wamekomaa kisiasa  na wamekuwa mabalozi wa amani msimu mzima.

Halikadhalika,aliwataka vijana kuendelea kudumisha amani hiyo huku akiwashauri kuwapokea viongozi wote waliochaguliwa kwa manufaa ya maendeleo na ukuaji wa uchumi wa taifa hili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *