Baraza la maimamu kaskazini mwa bonde la Ufa limewapongeza wakenya kwa ukomavu wao kutekeleza jukumu lao la kupiga kura kwa amani,kupokea matokeo hayo ya uchaguzi mkuu pamoja na uamuzi wa mahakama ya juu nchini kwa amani na utulivu.
Akiongea mjini Eldoret,mwenyekiti wa baraza hilo Sheikh Abubakar Bini alisema kwamba ni hatua nzuri na yastahili sasa wakenya kurejelea shughuli zao za maisha na ujenzi wa taifa na uchumi wa nchi.
Wakati huo,aliwataka wanasiasa na viongozi wote waheshimu uamuzi wa wakenya kwa kuzingatia njia ya sheria na za kikatiba ndipo malilio yao yaweze kusikizwa.