ASKOFU KIMENGICH:Wahakikishieni wakenya uchaguzi huru

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ameitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Iebc kuchukua hatua za kufanya uchaguzi huru na wa haki ifikapo uchaguzi mkuu ujao wa Agosti 9 mwaka huu.


Akiongea afisini mwake mjini Eldoret,askofu Kimengich alisema wakenya wameweka imani yao yote kwa tume hiyo na hivyo yapasa tume hiyo isisite kutekeleza jukumu lake akidai haipaswi kuonenkana kuwa haina mwelekeo wowote.


Askofu Vilevile aliwataka wanasiasa kuwa tayari kuyapokea matokeo ya kuanguka kwao na kufahamu kwamba kwenye kila shindano,lazima kuwepo mshindi na mshindani na lazima shughuli za kawaida kuendelea.


Aliwarai wakenya kudumisha amani kabla,wakati na hata baada ya uchagzu mkuu akiwakumbusha kuwa uchaguzi ni wa siku moja tu ila maendeleo na shughuli za ujenzi wa taifa zitasalia mikononi mwao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *