Washukiwa wawili wa wanaoaminika kuhusika kuirushia mawe gari ya mwaniaji kiti cha ugavana katika kaunti ya Uasin Gishu Zedekiah Bundotich maarufu Buzeki wametiwa mbaroni na maafisa wa polisi mjini Eldoret.
Akithitibitisha haya,naibu kamanda wa polisi kaunti ya Uasin Gishu Zacheaus Nge’no amedokeza kuwa wawili hao wanazuliliwa kwenye kituo cha polisi cha Central Eldoret na pindi uchunguzi utakapo kamilika watifikishwa mahakama kuhusu kisa hicho.
Aidha,Naibu huyo aliwataka wenyeji kuwa watu wa kuvumiliana na viongozi wa kisiasa wanapoendelea na kampeni zao waweze kuwapa nafasi ya kuuza sera zao bila ya kuvuruga akiwakumbusha kuwa wao ndio wtakao amua ni kiongozi yupi wanataka kumchagua ifikapo Agosti tisa mwaka kwenye uchaguzi mkuu.