viongozi wa dini la kiislamu:MAGOHA AOMBE MSAMAHA WAISLAMU

Viongozi wa dini la kiislamu kaskazini mwa bonde la Ufa wametoa makataa ya siku saba kwa waziri wa elimu nchini Profesa George Magoha kuiomba jamii la kiislamu msamaha la sivyo watakwenda kumshinikiza angatuke mamlakani.


Wakiongozwa na sheikh Abubakar Bini Viongozi hao walidokeza kuwa waziri magoha anastahili kuwa mtu wa kuigwa na walimu na siyo kutoa matamshi ya chuki na kidini kwa hili wakisema sharti hatua za haraka zichukuliwe za yey kuomba msamaha.


Wakizungumza mjini Eldoret,viongozi hao walidokeza kuwa kila mkenya anayo haki ya kuabudu na dini hiyo iwao inaruhusu kuwepo mavazi rasmi basi waweze kupewa heshima zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *