Idara ya afya ya umma kaunti ya Uasin Gishu imepiga marufuku kuanikwa kwa nafaka zozote mjini eldoret kutokana na kile inachosema ni kuhatarisha usalama wa vyakula hivyo.
Hatua inajiri siku moja tu baada ya maafisa wa polisi kumnasa mtu mmoja akiwa ameanika zaidi ya magunia 100 za ngano iliyooza karibu na maghala ya mazao na nafaka nchini NCPB mjini eldoret.
Waziri wa kilimo kaunti ya kilimo kaunti ya Uasin Gishu Samwel Yego amesema watahakikisha agizo la wizara ya afya limetelezwa kikamilifu.