Viongozi wa kisiasa kutoka eneo la Kapedo kaunti ya Turkana na maeneo jirani wamewashutumu vikali maafisa wa usalama wanaoendesha oparesheni ya kuwakabili wezi wa mifugo kwa kile wamesema ni kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia. Wakiongozwa na mbunge wa Tiaty William Kamket, viongozi hao wamemtaka waziri wa masuala ya ndani Fred Matiangi kusitisha mara moja oparesheni hiyo na badala yake kupisha mazungumzo.
Kwa upande wake seneta wa kaunti ya Pokot magharibi amedai mbinu inayotumika na vikosi vya usalama haiwezi kurejesha amani kwa maeneo yaliyoathirika.
Kauli za viongozi hao zinajiri wakati watu sita washukiwa wa wizi wa mifugo wameuawa wakati wa oparesheni iliyoanza hiyo jana kufuatia agizo lililotolewa na waziri wa masuala ya ndani Fred Matiang’i kufuatia kuuawa kwa afisa wa ngazi ya juu wa GSU Jumapili iliyopita.