Serikali kutoa usaidizi kwa Waathiriwa wa mafuriko

Waziri wa ugatuzi nchini Eugene Wamalwa amesema serikali imejitolea kuwapa msaada waathiriwa wa mafuriko kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.

Wamalwa anasema wakazi wengi hasa wanaoishi karibu na maeneo ya maziwa kama vile Nakuru, Bogoria, Baringo na Viktoria wamelazimika kuhama makwao baada ya kuongezeka kwa kiwango cha maji katika maziwa hayo na kusababisha mafuriko.

Wakati uo huo waziri huyo ameahidi waathiriwa kuwa serikali ya kitaifa kwa ushirikiano na zile za kaunti zinaendelea kuweka mikakati kuzuia kutokea kwa janga lolote. Haya yanajiri huku miundomsingi hususan barabara zikiharibika sehemu ambazo zimeshuhudia mafuriko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *