KEBS yanasa Magunia 993 ya mchele ilioharibika

Maafisa kutoka shirika la ukadiriaji ubora wa bidhaa (KEBS) imenasa Magunia 993 ya mchele ulioharibika wenye thamani ya shilingi milioni mbili nukta tatu mjini OrtumĀ  kaunti ya Pokot magharibi.

Inaarifiwa kuwa maafisa hao kwa ushirikiano na polisi wa eneo hilo walinasa mchele huo uliokuwa umepakiwa kwenye magunia madogo ya kilo 25 na ulikuwa unapakiwa upya kabla ya kuuziwa wananchi.

Shirika hilo aidha limeonya kuwa ni hatia kwa yeyote kuuza bidhaa zilizoharibika na kusema kuwa waliokamatwa watagharamia shughuli nzima ya kuuharibu mchele ulionaswa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *